Mshindi wa 2019
AISHA BAKARY

Jopo la majaji lilipokaa na kumuandaa mshindi Aisha alisimama kama mshindi wa thamani. Historia yake ndiyo iliyompa nafasi isiyo ya kawaida ya kukidhi malengo yetu ya kuchaguliwa kuwa mshindi wa mwaka 2019.

Kuishi katika nchi ya kiislam ambayo wanaume ndiyo watunga shaeria.ni vigumu kwa mwanamke kufanya kazi.Aisha siyo amefanya kazi zake za kila siku, bali amefanya biashara ambayo hamna mwanamke aliyewahi fanya kabla ndani ya visiwa vya Zanzibar. Kazi ya DJ ni kazi yenye misukosuko mingi, lakini hakuwaza kushindwa aliendelea hata alipokuwa haoni njia.alifanya kazi juu zaidi.
Na leo anafanya kama Dj wa kwanza mwanamke visiwani Zanzibarchini ya Hijab DJ .

Aisha amefanikiwa kuwatia moyo wanawake wengine wanaotamani kuwa Dj. Hapo zamani hawakuwa na nafasi ya kufanya hivyo.

Aisha ni mshindi wa thamani. Kazi yake inafaa sana kwa maono ya tuzo ya mwanamke mwenye ubaadae.Aisha atakuwa mshindi wa kuangaliwa kwa washiriki wajao.

Aisha Bakary DJ-ing
Aisha Bakary with her mixing table

Ni kazi sana kuwa Dj mwanamke hapa Zanzibar. Ukizingatia 99% ya watu wake ni waislam. Dini siyo vile unavyoonekana bali ni kile unachokiamini. Nilipata jumbe mbaya lakini najiamini na sikati tamaa kwenye ndoto zangu. Mpaka zitimie.

Aisha Bakary, lebo ya Hijab DJ.