Kuhusu
mwanamke mwenye ubaadae

Asili yake

Mwaka 2018 nilikutana na Lilian Okhobe ndani ya Zanzibar.na aliniambia kuhusu ndoto aliyonayo ya kuanzisha ufugaji wa kuku.ili aweze kufanya biashara.sasa jengo limeshajengwa na Lilian ameshaingia katika ulimwengu wa biashara.alikuwa na ndoto ya kufanya biashara kubwa ili aweze kuajiri wanawake wenzake.mipango tuliyoindeleza ya kutengeneza mabanda ya kuku ndiyo yaliyonifanya nijizatiti katika kusherekea maisha ya wanawake wachache ndani ya .Zanzibar.ambao wanafanya vitu vya kipekee. Wale wanaojihusisha katika utalii,viongozi wa jamii, wajasiriamali, wafanyabiasharana wale wenye chachu ya maendeleo katika jamii zao.vikundi vya wanawake,kukufanya kazi za watoto,za wazee na nyingine nyingi zinazoleta maendeleo katika jamii.hawa wanawake wanatakiwa kutambulika ili iwe njia ya kuvumbua na kuendeleza kazi za mwanamke anayetia moyo na kuigwa katika jamii.hilo ndiyo sababu ya kuundwa mwanamke wa ubaadae.

John John Bruseth, mwanzilishi

Maono yetu

Tunatoa Tuzo kwa mwanamke wa mwaka na kumsaidia kufikia mafanikio yake.

Maono yetu kuifanya tuzo hiyo ijulikane Zanzibarkama tuzo yenye thamani. Yenye majukumu ya kutengeneza wanawake wa kuigwa na wenye kutia moyo wengine ili wawe wajasiriamali,waanzishe biashara,wawe viongozi,au kuongoza nafasi zilizoshikiliwa na wanaume.

Lengo letu

Usawa wa kijinsia ni moja kati ya mikakati 17 ya umoja wa mataifa ili kuibadilisha dunia.

Mnamo 2015, nchi ziliasili 2030 agenda za maendeleo na mikakati 17 ya kukuza uchumi. Mapema mwezi wa nane 2015nchi wanachama 193walikuja na agenda ya kubadlisha dunia. Agenda 2030kwaajili ya maendeleo. Lengo namba tano inazungumzia usawa wa kijinsia likiwa na dhumuni la kuwezesha wanawake na wasichana. Pia inasema kwamba, Usawa wa kijinsia siyo tu ni haki za binadamu bali pia ni msingi wa amani, ustawi na kuhimili dunia.

Lengo namba 5
Usawa wa kijinsia

Usawa wa kijinsia siyo tu ni haki za binadamu bali pia ni msingi wa amani,ustawi na kuhimili dunia.

Tembelea UN (UMOJA WA MATAIFA)

Washirika (ubia)

ID Leadership

ID Leadership

Dream Big Women Academy Logo

Dream Big Women Academy

Chuo cha wanawake wenye ndoto kubwa Nia yetu ni kumwezesha mwanamke ,kumfundisha ili aweze kutengeneza biashara ndogondogoili kujiongezea kipato. Tunatoa fursa kwao ili waweze kuinuka kwaajili yao na familia zao na jamii kwa ujumla Tafadhali Tembelea: www.dreambigwomenacademy.no

Johooo Foundation Logo

Johoo Foundation

Msingi wa johoo Ni taasisi isiyo ya kiserikali ya Norway.yenye lengo la kusaidia wanawake na wasichana Zanzibar.kwa kuwafundisha ufugaji wa kuku wa mayai na kuwapa mitaji ili ili waweze kufuga kuku wao Tunawasaidia kwa ubaadae wao na watoto wao.nyumba ya kuku ya lilian ni mfano hai. Nyumba hizo zilijengwa kwa msaada wa johoo . pia tunajenga nyumba kwaajili wanawake 20 unguja ukuu.wanawake wote wanapata fedha kutoka johoo.

Symfoni Logo

Symfoni Next